1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Mamia ya wahamiaji wamekufa robo ya kwanza ya 2023

12 Aprili 2023

Umoja wa Mataifa umesema leo robo ya kwanza ya mwaka huu imekuwa ni kipindi kibaya kabisa kwa wahamiaji wanaofanya safari za hatari katika bahari ya Meditrenia kuliko kuliko ilivyotokea mwaka 2017.

https://p.dw.com/p/4PxzL
Wahamiaji baada ya kuwasili Italia
Wahamiaji wengi kutoka Afrika huvuka bahari ya Mediterannia kujaribu kuingia UlayaPicha: Marco Zac/NurPhoto/picture alliance

Umoja wa Mataifa umesema kuanzia mwezi Januari hadi Machi mwaka huu 2023 watu 441 wamepoteza maisha kwa kujaribu kufika barani Ulaya kupitia bahari ya Mediterania.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM limesema kucheleweshwa kwa operesheni za uokozi za serikali ni chanzo kikuu cha maafa ya baharini kwa watu wanaotoka eneo la Kaskazini mwa Afrika.

IOM imesema idadi kamili ya vifo huenda ikawa ya juu kuliko watu hao 441 waliotajwa kufa katika miezi mitatu ya kwanza mwaka huu.

Mkuu wa IOM Antonio Vitorino, amesema maafa yanayotokea katika bahari ya Mediterania hayawezi kuvumilika.