1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN kuanza kutoa chanjo ya dharura kwa ugonjwa wa surua DRC

26 Septemba 2019

Umoja wa Mataifa kuanza kutoa chanjo ya dharura dhidi ya ugonjwa wa Surua katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

https://p.dw.com/p/3QHV6
Impfung gegen Masern
Picha: Imago/Xinhua

Umoja wa Mataifa umesema jana kwamba utafanya kampeni ya dharura ya kutoa chanjo katika majimbo sita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupambana na mripuko wa ugonjwa wa surua ambao umesababisha vifo vya watu wapatao 3,600 tangu ulipoanza mwanzoni mwa mwaka huu.

Shirika la Afya Duniano, WHO, limesema tangu mwanzo wa mwaka hadi Septemba 17, serikali imerekodi visa 183,000 vinavyoweza kuwa vya ugonjwa wa surua, ambao unaweza kuzuilika kwa chanjo.

Shirika hilo limesema watu 3,667 wameshafariki, wengi wao wakiwa watoto. Idadi hiyo ni kubwa zaidi kuliko ya watu waliokufa kutokana na ugonjwa wa Ebola katika maeneo ya mashariki mwa Kongo.

Shirika hilo limesema, kampeni hiyo inakusudia kutoa chanjo kwa takriban watoto 825,000 katika mikoa 24, katika kipindi cha siku tisa.