1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSyria

UN inasaka msaada wa dola bilioni 4 kuwasaidia raia wa Syria

23 Machi 2024

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa misaada ya dola bilioni 4 ili kuokoa maisha ya watu milioni 10 nchini Syria ikisema mzozo wa kibinadamu uliosahaulika nchini humo, unasalia kuwa moja kati ya majanga makubwa duniani.

https://p.dw.com/p/4e35p
Raia wa Syria waliokimbia makaazi yao wakiwa nje ya mahema yaliyoharibiwa kutokana na mvua
Raia wa Syria waliokimbia makaazi yao wakiwa nje ya mahema yaliyoharibiwa kutokana na mvuaPicha: Anas Alkharboutli/dpa/picture alliance

Mratibu mkaazi wa ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu nchini Syria Adam Abdelmoula ametoa mwito huo siku chache baada ya Syria kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 13 ya mzozo huo uliosababisha vifo vya karibu watu nusu milioni na kuacha sehemu kubwa ya nchi ikiwa imeharibika.

Soma pia: Iraq yawarejesha makwao wakimbizi 625 kutoka kambi ya Syria

Abdelmoula amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa, jamii ya kimataifa kutochukua hatua kutasababisha mateso zaidi kwa raia wa Syria.

Takriban watu milioni 16.7 wanahitaji msaada wa kibinadamu, idadi hiyo ikiongezeka kutoka watu milioni 15.3 mwaka uliopita.

Zaidi ya watu milioni 7 wameachwa bila maakazi rasmi huku wengine wakitafuta hifadhi katika nchi nyingine ikiwa ni pamoja na Jordan, Lebanon na Uturuki.