1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU na Misri zaingia makubaliano biashara ya dola bilioni 1.1

29 Juni 2024

Umoja wa Ulaya na Misri leo hii zimesaini makubaliano ambayo yatawezesha umoja huo kuwekeza hadi dola bilioni 1.1 ikiwa ushirikiano wa kimkakati katika taifa hilo la kiarabu lenye idadi kubwa ya watu.

https://p.dw.com/p/4hfLS
Kamishna wa Umoja wa Ulaya von der Leyen na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi mjini Cairo
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der Leyen na rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi 17 Machi 2024 huko Cairo, Misri.Picha: Dirk Waem/dpa/Belga/picture alliance

Makubaliano hayo ya kifedha ni sehemu ya mwanzo ya ahadi katika kitita cha dola bilioni 4, ambacho Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya, Ursula von der Leyen alikitangaza mwezi Machi.

Kwa mujibu wa halmashauri hiyo, fedha hizo zitatumika katika uwekezaji katika sekta kadhaa ikiwemo ya nishati safi. Mkataba huo umetiwa saini na Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya, Valdis Dombrovskis na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Misri Rania al-Mashat katika kongamano la siku mbili la uwekezaji la Umoja wa Ulaya na Misri la mjini Cairo.

Misri, ambayo inatoa hifadhi kwa takriban wakimbizi na wahamiaji milioni 9, inaathiriwa na vita vya miezi kadhaa kati ya Israel na Hamas katika eneo jirani la Ukanda wa Gaza.