1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaKenya

Umoja wa Ulaya yaahidi kuongeza uwekezaji nchini Kenya

22 Februari 2023

Umoja wa Ulaya umesema utatanua uwekezaji wake nchini Kenya kwa mamilioni ya dola ukilenga kuimarisha uhusiano na taifa hilo la Afrika Mashariki katikati mwa ushindani kutoka China.

https://p.dw.com/p/4NomR
Afrika, Kenia | Lake Turkana Wind Project Kenya, Ngong Power Station
Picha: Dai Kurokawa/epa/picture alliance

Akizungumza Jumanne katika siku ya kwanza ya Jukwaa la Biashara kati ya Kenya na Umoja wa Ulaya mjini Nairobi, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Kenya Henriette Geiger, alisema uwekezaji huo utazilenga sekta ambazo bado hazijaimarishwa.

Geiger amesema mikataba mipya itakayotiwa saini ni sehemu ya mkakati wa Umoja wa Ulaya wa kukusanya takribani dola bilioni 340 kusaidia sekta ya miundombinu ya umma na binafsi, kote ulimwenguni ifikapo mwaka 2027.

Miongoni mwa makubaliano yatakayofikiwa ni pamoja na ahadi ya mchango wa dola milioni 200 kuisaidia benki ya biashara na maendeleo inayoendeshwa kwa pamoja na mataifa kadhaa ya Afrika. 

Benki hiyo imekuwa ikizisaidia kampuni za mataifa ya mashariki na kusini mwa Afrika zilizoathirika na vita vya Ukraine