1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Makubaliano ya EU ya kuishtaki Urusi kwa uhalifu wa kivita

4 Machi 2023

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen ametangaza makubaliano ya uanzishwaji wa Kituo kipya cha Kimataifa cha Mashtaka ya Uhalifu wa Uchokozi (ICPA) yatakayotiwa saini wikiendi hii.

https://p.dw.com/p/4OFyV
Ukraine, Kiew | Ursula von der Leyen
Picha: Efrem Lukatsky/AP/picture alliance

Von der Leyen amesema hatua ya kwanza muhimu itakuwa kuiwajibisha Urusi na Rais Vladimir Putin kwa uhalifu wa kutisha dhidi ya Ukraine na kufanya kila liwezekanalo ili kuwafikisha wahusika mahakani.

Rais huyo wa Tume ya Ulaya amebainisha pia kuwa kuna ushahidi unaoongezeka wa mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya raia, mateso na unyanyasaji wa kijinsia.

Soma pia:Putin 'sio mshukiwa pekee' katika uhalifu nchini Ukraine 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema suala kuu ni kubaini jukumu la Urusi na viongozi wake kwa uchokozi na ugaidi dhidi ya Ukraine.