1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa ulaya wasitisha mazungumzo na Iran

23 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEiQ

Paris:

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Ufaransa, inasema dola za Ulaya zimefuta mazungumzo yaliopangwa tarehe 31 ya mwezi huu wa Agosti na Iran, ili kuiraia isitishe mpango wake wa kinuklea. Msemaji wa wizara hiyo Jean-Baptiste Mattei alisema mazungumzo hayo sasa hayawezi kuendelea kwa sababu Iran imeanza tena kazi ya kurutubisha Uranium, kinyume na ahadi ya kusita kufanya hivyo ili mazungumzo yaendelee. Umoja wa Ulaya na Marekani zina shuku kuwa Irak inajaribu kisiri siri kuunda silaha za kinuklea. Iran lakini inasema inataka teknolojia ya nuklea kwa ajili tu ya mahitaji ya nishati.