1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Umoja wa Ulaya wasikitishwa na mauaji ya raia 1,000 Darfur

Sylvia Mwehozi
13 Novemba 2023

Umoja wa Ulaya umeelezea kushtushwa na ripoti za mauaji ya watu zaidi ya 1,000 katika eneo la Darfur Magharibi mwa Sudan. Idadi hiyo ni kubwa kuliko iliyotolewa awali na shirika la UNHCR ya watu 800.

https://p.dw.com/p/4YjAR
Wakimbizi-Sudan
Wakimbizi wa Sudan waliokimbilia mapiganoPicha: Marie-Helena Laurent/WFP/AP/picture alliance

Umoja wa Ulaya umeelezea kushtushwa na ripoti za mauaji ya watu zaidi ya 1,000 katika eneo la Darfur Magharibi mwa Sudan. Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alisema jana kwamba mauaji hayo ya hivi karibuni yanaonekana kuwa sehemu ya kampeni pana ya safisha ya kikabila iliyoendeshwa na wanamgambo wa kundi la RSF kwa lengo la kutokomeza jamii ya Masalit ambayo sio Waarabu kutoka Darfur Magharibi.UN: Nusu ya raia wa Sudan wanahitaji msaada wa kiutu

Taarifa ya Umoja wa Ulaya inasema inazo ripoti za mashahidi wa kuaminika za mauaji hayo huko Ardamta, magharibi mwa mkoa wa Darfur ndani ya siku mbili. Umoja huo umeonya juu ya hatari ya mauaji mengine ya halaiki mkoani Darfur.

Idadi hiyo ni kubwa kuliko iliyotolewa awali na shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR ya watu 800.