1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wakutana kutafuta msimamo wa pamoja kuhusu Kosovo

14 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cbib

Baada ya kutia sahihi mkataba wa mageuzi mjini Lisbon,viongozi wa Umoja wa Ulaya watakutana mjini Brussels, kujaribu kupata msimamo wa pamoja kuhusu jimbo la Serbia la Kosovo.

Raia wa asili ya Albania ambao ndio wengi katika jimbo hilo wanataka kujitenga kutoka kwa Serbia.Hatua yao hiyo inaungwa mkono na Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani.Hata hivyo baadhi ya vigogo katika Umoja wa Ulaya ,akiwemo kamishna anaehusika na kupanuliwa kwa Umoja huo-Olli Rehn, wanahofu kuwa suala hili laweza likawapa msukumo wazalendo wa Kiserb katika uchaguzi ujao wa urais utakaofanyika mwezi januari.Urusi nayo inapinga kwa jimbo hilo la kupewa uhuru. Sintofahamu kati ya Moscow na mataifa ya Ulaya Magharibi ilisababisha kukwama kwa mazungumzo ya umoja wa Mataifa.Mazungumzo yalimalizika wiki hii.