1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waimarisha vikwazo zaidi kwa Syria

15 Novemba 2011

Umoja wa Ulaya umeimarisha vikwazo dhidi ya utawala wa rais wa Syria bashar al Assad katika hatua ya kupinga ukamizaji wake dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali.

https://p.dw.com/p/13AYs
Rais wa Syria Bashar al Assad ambaye utawala wake umeongezewa vikwazo zaidi na umoja wa ulaya.Picha: picture-alliance/dpa

Umoja wa Ulaya umeimarisha vikwazo dhidi ya utawala wa rais wa Syria Bashar al Assad katika hatua ya kupinga ukandamizaji wake wa miezi kadha sasa dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali. Mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka mataifa 27 ya umoja wa Ulaya wamerefusha adhabu kwa watu 18 zaidi wanaohusiana na ukandamizaji huo. Hatua hizo ni pamoja na uwezekano wa kuzuwia mali zozote zilizoko katika umoja wa Ulaya. Kundi hilo la mataifa limeweka tayari vikwazo vya mafuta kutoka Syria. Mawaziri hao pia wameamua kufuta mikopo kwa Syria iliyotolewa na benki ya rasilmali ya umoja wa Ulaya. Siku ya Jumamosi , umoja wa nchi za kiarabu, Arab League umeisitisha Syria kuhudhuria mikutano yake na kutangaza mipango ya kuiwekea vikwazo hadi pale itakapotekeleza mapendekezo ya mpango wa amani wa umoja huo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Syria ameiita hatua ya kusitishwa uanachama kuwa ni kinyume cha sheria na ya hatari.