EU yaidhinisha kurefushwa muda wa vikwazo dhidi ya Urusi
27 Januari 2025Matangazo
Mawaziri wa mambo ya Nje wa umoja huo walifikia uamuzi huo walipokutana leo mjini Brussels Ubelgiji.
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas amesema hatua hii itaendelea kuinyima Moscow mapato ya kufadhili vita vyake.
SOma pia:Ukraine yaishambulia Urusi kwa droni 121
Hata hivyo kulikuwa na wasiwasi kwamba Hungary ingelipinga hatua hiyo, lakini taarifa zimeeleza kuwa Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban alifikia makubaliano na wenzake wa Ulaya na kuamua kuunga mkono mpango huo.