Umoja wa Ulaya waapa kujibu ushuru wa Marekani
11 Februari 2025Matangazo
Katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake mjini Brussels, Bibi Von der Leyen amesema Umoja wa Ulaya utachukua hatua nzito za kujibu mapigo, akiahidi kwamba kanda hiyo italinda maslahi yake ya kiuchumi dhidi ya kile amekitaja kuwa"ushuru usio na msingi". Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza jana Jumatatu ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa zote za chuma na alumini kutoka mataifa ya kigeni akitumai kuyalinda makampuni ya ndani dhidi ya ushindani kutoka nje. Hata hivyo, hatua kama hizo wakati wa utawala wake wa awamu ya kwanza ziliteteresha mahusiano ya Washington na washirika wake na kupandisha bei ya bidhaa za chuma na alumini.