1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUbelgiji

Umoja wa Ulaya waahidi kusimama na Ukraine bila kuchoka

10 Februari 2023

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamemhakikishia Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuwa Ulaya itaendelea kumuunga mkono katika vita vyake dhidi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4NK1i
Belgien Brüssel | EU-Gipfel | Rede Wolodymyr Selenskyj im EU-Parlament
Picha: Kenzo Tribouillard/AFP/Getty Images

Hata hivyo wametoa ahadi chache madhubuti baada ya mkutano wao wa kilele mjini Brussels.

Katika taarifa iliyotolewa mapema leo, Umoja wa Ulaya umesema utasimama na Ukraine bila kuchoka. Viongozi hao wa Ulaya wamesema vita vya Urusi, ambavyo vimedumu kwa mwaka mmoja sasa, vimesababisha mateso na uharibifu mkubwa kwa Ukraine na watu wake. Olaf Scholz ni Kansela wa Ujerumani.

"Vita ambavyo Urusi inashiriki dhidi ya Ukraine, ni vita ambavyo vimetuathiri sote, na vitatuathiri sote ulimwenguni kutokana na changamoto za kibiashara na kiuchumi, lakini pia itaathiri zaidi kutokana na kuguswa kwetu na uchangiaji kwa vitendo kwa Ukraine, " amesema Scholz.

Wameitaka Urusi kusitisha vita hivyo mara moja. Hata hivyo, viongozi hao walijiepusha na masuala kama vile matumizi ya fedha zilizokamatwa za Urusi kutumika katika ujenzi mpya wa Ukraine.