1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya na Uingereza zapiga hatua katika mazungumzo

19 Machi 2018

Uingereza na Umoja wa Ulaya zimekubaliana kuhusu masuala kadhaa kuhusu Uingereza kujitenga na Umoja huo, ikiwemo masharti ya kipindi cha baada ya utengano

https://p.dw.com/p/2uaWh
Belgien  Europa Brexit Michel Barnier David Davis
Picha: picture-alliance/AP Photo/V. Mayo

Uingereza na Umoja wa Ulaya zimepiga hatua nzuri katika mazungumzo kuhusu Brexit. Pande zinazoshiriki mazungumzo zimekubaliana kuepuka mgogoro wa mpaka kati ya Ireland Kaskazini na mkoa wa Ireland kaskazini nchini Uingereza. Hayo yanajiri kabla ya mkutano muhimu wa kilele wiki hii ambapo Uingereza inatumai itafikiana na Umoja wa Ulaya kuhusu kipindi cha baada ya utengano.

Uingereza na Umoja wa Ulaya zimekubaliana kuhusu masuala kadhaa kuhusu Uingereza kujitenga na Umoja huo, ikiwemo masharti ya kipindi cha baada ya utengano ambacho kitadumu hadi mwisho wa mwaka 2020. Hayo yamesemwa na mshauri mkuu wa Umoja wa Ulaya, Michel Barnier.

Umoja wa Ulaya inataka kuukamilisha mkataba wa Uingereza kujiondoa ifikapo mwezi Oktoba wakati nchi hiyo ikijiandaa kujiondoa rasmi mwezi Machi mwaka 2019.

Kuhusu Ireland na Ireland Kaskazini, tumekubaliana kuwa lazima tume na masuluhisho ya kweli na yanayowezekana ili kuepuka mgogoro wa mpaka. Uingereza na Umoja wa Ulaya zimekubaliana leo kuhusu namna ambavyo masuala ya Ireland yatakavyoshughulikiwa

Mkataba huo utajumuisha masharti ya Uingereza kujiondoa na maelezo ya kipindi cha kujiondoa, ambayo yatayapa makampuni na raia uhakikisho ya hali kuwa saw ahata baada ya utengano na kutoa muda w akutosha kwa Uingereza kuweka mikakati yao sawa baada ya kujiondoa.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa MayPicha: picture alliance/dpa/J. Brady/PA Wire

Mshauri mkuu wa Uingereza katika mazungumzo hayo David Davis ameyapongeza makubaliano hayo kuhusu kipindi cha mpito.

"Moja kati ya malengo yetu makuu kwenye hotuba yangu ni kwamba sauti ya Uingereza itaweza kusikika wakati wa kipindi hiki na kuhakikisha masilahi yetu yamelindwa. Hili linatimiza lengo hilo."

Pande hizo mbili pia zimekubaliana kuepuka utata wa mpaka kati ya mkoa wa Ireland kaskazini wa Uingereza na Ireland Kaskazini ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland, Simon Coveney, amesisitiza kuwa suala hilo la mpaka linasalia kuwa hoja muhimu kwa pande zote mbili pamoja na uimarishaji wa ushirikiano thabiti miongoni mwa wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Nchi 27 ambazo zimesalia kuwa wanachama wa Umoja wa Ulaya zinasema Uingeraza lazima ikubaliane na masharti kuhusu Ireland Kaskazini kabla itie saini mkataba kamili wa utengano wao na mazungumzo ya kibiashara yanayotarajiwa mwezi Aprili.

Uingereza imekuwa ikitaka suala kuhusu kipindi cha baada ya utengano litatuliwe ifikapo wakati viongozi wa Umoja wa Ulaya watakapokutana wiki hii mjini Brussels kati ya tarehe 22 na 23, ili kutoa uhakikisho kwa wafanya biashara ambao wana wasiwasi wa ukosefu wa mipango ya kiuchumi baada ya Brexit.

Mazungumzo yamelenga kufikia maelewano kuhusu kipindi cha mpito cha baada ya utengano, ambapo Uingereza itafuata sheria za Umoja wa Ulaya hadi pale itakapojitenga kikamilifu na umoja huo mwezi Machi mwaka 2019. Au hadi mwisho wa mwaka 2020 kama njia ya kurahisisha mambo kutokana na mshtuko wa utengano huo.

Mwandishi: John Juma

Mhariri: Mohammed Khelef