Umoja wa Ulaya kushirikiana zaidi
18 Juni 2010Matangazo
Kwenye mkutano wao mjini Brussels, viongozi wa taifa na serikali kutoka nchi wanachama 27 wamekubali pia kuchapisha matokeo ya uchambuzi uliofanywa kuhusu benki 25 kubwa kabisa za Ulaya,juu ya uwezo wa benki hizo kukabiliana na mizozo ya kifedha katika siku zijazo.
Viongozi hao wa Umoja wa Ulaya vile vile wamekubali kuanzisha mpango wa kuzitoza kodi maalum benki za Ulaya. Na katika mkutano wa kundi la nchi 20 zilizoendelea na zinazoinukia kiuchumi, utakaofanywa nchini Kanada baadae mwezi huu, watapendekeza kuzitoza benki kodi kwa kila biashara ya fedha. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema, Umoja wa Ulaya utaimarisha ushirikiano wake. Wanachama wote wametambua kuwa ni lazima kushirikiana zaidi.
Mwandishi:P.Martin/ZPR