1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Umoja wa Ulaya kuimarisha uhusiano na Ufilipino

31 Julai 2023

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen aliye ziarani nchini Ufilipino amesema wako tayari kutanua ushirikiano na serikali ya Manila katika eneo la usalama wa usafiri baharini.

https://p.dw.com/p/4Uank
Ursula von der Leyen besucht Philippinen
Picha: Rolex dela Pena/Reuters

Von der Leyen alitowa kauli hiyo baada ya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Ferdinand Marcus Jr. mjini Manila, ambapo wawili hao walijadiliana masuala kadhaa yakiwemo ya usalama, biashara na mabadiliko ya tabianchi.  

"Usalama wa Ulaya na ule wa Bahari ya Hindi na Pasifiki havitenganishiwi. Umoja wa Ulaya umekuwa ukiunga mkono mazingira ya uhuru na ya wazi ya kanda hiyo, kwa sababu eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki lisilo na vitisho ni muhimu kwa uthabiti wetu, amani yetu na ustawi wa watu wetu." Alisema kiongozi huyo wa Umoja wa Ulaya.

Soma zaidi: Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen ameanza ziara kuelekea mataifa manne ya Amerika Kusini

Kwa miaka kadhaa sasa, Ufilipino imetumbukia kwenye uhasama na China kutokana kuwania udhibiti wa sehemu ya Bahari ya Kusini mwa China, ambayo Beijing inadai umiliki kamili.