1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Matiafa wataka jeshi lipelekwe Haiti

25 Aprili 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amehimiza kupelekwa mara moja kwa jeshi la kimataifa nchini Haiti ili kudhibi machafuko yanayoongezeka

https://p.dw.com/p/4QWdE

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amehimiza kupelekwa mara moja kwa jeshi la kimataifa nchini Haiti ili kudhibi machafuko yanayoongezeka ambayo yanafanywa na magenge ya uhalifu na mgogoro mbaya kabisa wa haki za binaadamu kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika miongo mingi. Guterres ameonya katika ripoti kuwa ukosefu wa usalama katika mji mkuu Port-au-Prince umefikia viwango vinavyofanana na nchi zinazokumbwa na vita. Guterres amesema tangu mwanzo wa 2023, polisi 22 wameuawa na magenge ya uhalifu na matukio hayo yanatarajiwa kuongezeka kwa kasi kama hakutakuwa na juhudi maradufu za kutoa vifaa na mafunzo kwa polisi na kuwaajiri kazi maafisa wapya pamoja na kuimarisha mazingira ya kazi. Tangu mauaji ya Rais Jovenel Moise Julai 2021, magenge ya Haiti yameendelea kuwa na nguvu. Guterres alitoa ombi la dharura la kupelekwa vikosi maalum katika taifa hilo la Amerika Kusini Oktoba mwaka jana kufuatia ombi la Rais Ariel Henry na Baraza la Mawaziri la nchi hiyo. Lakini hakuna nchi iliyojitokeza kuongoza kikosi hicho na badala yake, jamii ya kimataifa imekuwa ikiweka tu vikwazo na kutuma vifaa vya kijeshi na raslimali nyingine.