1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UMOJA WA MATAIFA:Ujumbe wa Umoja wa Mataifa umefunga safari ...

12 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEEL
kuelekea Afrika kuchunguza kama kinakiukwa kikwazo cha silaha ilichoekewa Somalia. Stefan Tafrov, balozi wa Bulgaria kwenye Umoja wa Mataifa, na mwanachama wa Baraza la Usalama, anaongoza ujumbe huo kwa siku 10, ambao uliondoka juma lililopita kukutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za kiarabu, Arab League, Bwana Amri Musa mjini Cairo, Misri. Kadhalika utakuwa na ziara ya Ethiopia, Jibuti, Yemen, Eritrea, Kenya na Italy, zamani dola ya kikoloni nchini Somalia. Ziara inafanyika kufuatia ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa wiki iliopita kuwa Somalia inatumiwa kama kituo na mtandao wa kigaidi wa Osama Bin Laden ambacho kundi lake ndilo lilianzisha mashambilizi ya mabomu mwaka mmoja uliopita nchini Kenya.