1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaeSwatini

Umoja wa Mataifa waitisha uchunguzi wa mauaji ya Eswatini

23 Januari 2023

Mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk ameitolea wito Eswatini kuchunguza haraka mauaji ya kikatili ya mwanasiasa maarufu wa upinzani na mwanasheria wa haki za binaadamu Thulani Maseko.

https://p.dw.com/p/4MZxH
Eswatini | 4.	Sicherheitskräfte in Manzini jagen Demonstranten
Picha: Adrian Kriesch/DW

Turk amesema Maseko alikuwa mpiganiaji mahiri wa haki za binadamu ambaye alihatarisha maisha yake ili kupaza sauti za wale ambao walishindwa kujisemea na ametaka uchunguzi huo ufanyike bila kuegemea upande wowote.

Maseko alipigwa risasi na kuuawa Jumamosi usiku na washambuliaji wasiojulikana nyumbani kwake Luhleko, umbali wa kilometa 50 kutoka mji mkuu, Mbabane. Alipigwa risasi kupitia dirishani akiwa ndani na familia yake.

Maseko alikuwa mwasisi wa kundi la Multi-Stakeholder Forum - MSF - muungano wa vyama vya upinzani, mashirika na makanisa.