Asili na mazingiraUkraine
Mataifa tajiri yaombwa kufanikisha mazungumzo ya mazingira
18 Novemba 2024Matangazo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye atahudhuria mkutano wa kilele wa G20 unaoanza leo Jumatatu huko Rio de Janeiro, amesema matokeo yenye mafanikio katika COP29 bado yanaweza kufikiwa, lakini yatahitaji uongozi na maelewano kutoka kwa nchi za G20.
Mazungumzo ya COP29 mjini Baku yamekwama licha ya wiki moja ya majadiliano, huku mataifa yakishindwa kukubaliana kuhusu mkataba wa dola trilioni 1 kwa ajili ya uwekezaji wa miradi ya hali ya hewa katika mataifa yanayoendelea.
Mbali na kiwango hicho, bado kuna mivutano pia kuhusu aina ya ufadhili na nani anayepaswa kutoa fedha hizo, huku nchi za Magharibi zikiitaka China na mataifa tajiri ya Ghuba kujiunga katika orodha ya wafadhili.