1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres: Tunisia iache kuwafukuza wahamiaji

2 Agosti 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa Tunisia kuacha kuwafukuza wahamiaji hadi katika maeneo ya mipaka ya jangwani.

https://p.dw.com/p/4Ug4K
Tunesien | Ausschreitungen in Sfax, Migranten
Picha: Hasan Mrad/ZUMA Wire/IMAGO

Guterres ametaka wale ambao tayari wamekwama katika mazingira magumu kuhamishiwa maeneo salama. Naibu msemaji wa Guterres, Farhan Haq amesema Umoja wa Mataifa una wasiwasi mkubwa kuhusu kufukuzwa kwa wahamiaji, wakimbizi na waomba hifadhi kutoka Tunisia hadi kwenye mipaka ya Libya na pia Algeria. Ameonya kuwa watu kadhaa wamefariki katika mpaka wa Tunisia na Libya, huku mamia ya wengine, wakiwemo wanawake wajawazito na watoto, wakiripotiwa kusalia katika hali mbaya sana bila chakula na maji. Katika siku za karibuni, mamia ya wahamiaji wamewasili kila siku nchini Libya baada ya kutelekezwa katika mpaka wa jangwa na vikosi vya usalama vya Tunisia. Hayo ni kwa mujibu wa walinzi wa mpaka wa Libya na wahamiaji wenyewe.