1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Wahamiaji zaidi wakimbilia Ulaya kupitia Mediterania

5 Julai 2024

Umoja wa mataifa na washirika wake wamesema wahamiaji zaidi kutoka barani Afrika wanakimbilia Ulaya wakitumia njia hatari ya Mediterania na jangwa la Sahara.

https://p.dw.com/p/4hw11
Mittelmeer | Flüchtlinge durch das Aurora-Rettungsschiff von Sea-Watch gerettet werden
Boti ya wahamiaji kama inavyoonekana pichani wakijaribu kukimbilia Ulaya kupitia bahari ya Mediterania, Agosti 18, 2023. Picha: Rebecca Berker/ROPI/picture alliance

Umoja wa mataifa na washirika wake wamesema wahamiaji na wakimbizi zaidi kutoka barani Afrika wanaelekea maeneo ya Kaskazini kuelekea bahari ya Mediterranea na Ulaya wakipitia njia hatari katika eneo la jangwa la Sahara.

Wamesema eneo hilo pia kunapatikana magenge ya uhalifu yanayoendesha matukio ya utumwa, kuwanyofowa viungo vyao vya mwili, ubakaji, kuwafanyia matukio mengine ya unyanyasaji pamoja na kuwateka nyara, wakidai kikombozi.

Ripoti iliyochapishwa Ijumaa hii na mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kushughulikia wakimbizi na wahamiaji imekadiria kwamba njia za ardhini zinazotumiwa na wakimbizi na wahamiaji barani Afrika kuelekea Ulaya ni hatari kama zilivyo njia za kupitia bahari ya Mediterrania.

Ripoti hiyo imesema vita vipya pamoja na ukosefu wa uthabiti katika mataifa kama Mali,BurkinaFaso na Sudan yamechangia ongezeko la idadi ya wakimbizi wanaofanya safari kuelekea bahari ya Mediterrania.