1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wasema Israel haizingatii ulinzi wa raia

19 Juni 2024

Afisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu inasema Israel haijatilia maanani ulinzi wa raia inapotumia mabomu yanayoelekezwa kulenga sehemu maalum katika vita vya Gaza.

https://p.dw.com/p/4hFId
Volker Türk
Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Türk.Picha: Jean-Noel Ba-Mweze/DW

Haya yalisemwa siku ya Jumatano (Juni 19) na Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Türk, mjini Geneva.

Türk alisema afisi yake imechunguza mashambulizi sita ya Israel katika Ukanda wa Gaza kati ya Oktoba 9 na Desemba 2.

Kauli ya mkuu huyo wa haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa ilitolewa, wakati kukiripotiwa mashambulizi ya angani ya Israel na mapigano kati ya vikosi vyake na wanamgambo wa Kipalestina huko Gaza.

Soma zaidi:Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aikosoa Marekani kwa kuzuia silaha

Mashuhuda na mashirika ya ulinzi wa kiraia katika Ukanda wa Gaza yameripoti mashambulizi ya mabomu ya Israel magharibi mwa Rafah ambapo maafisa wa afya wanasema kuwa mashambulizi hayo yamewauwa watu saba. 

Kwa upande mwengine, jeshi la Israel lilisema kwamba liko tayari kuwashambulia wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon kutoka kaskazini mwa Israel.