1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaonya kuhusu hali ya Gaza kujirudia nchini Lebanon

8 Oktoba 2024

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameonya kwamba mfumo wa kivita uliotumiwa na Israel na ambao ulisababisha maafa kwa idadi kubwa ya raia na uharibifu huko Gaza, sasa unajirudia nchini Lebanon.

https://p.dw.com/p/4lXvr
Lebanon | Milipuko kusini mwa Lebanon
Moshi unafuka kwa upande wa kusini mwa Lebanon kama unavyoonekana kutoka kaskazini mwa Israel, Jumatatu, Okt. 7, 2024Picha: Leo Correa/AP Photo/picture alliance

Maafisa hao wametoa pia wito wa kuchukuliwa hatua za kukomesha muendelezo wa mateso. Naibu mkuu wa Hezbollah Naim Qassem amesema hivi leo kuwa kundi hilo linaunga mkono juhudi za serikali ya Lebanon za kusitisha mapigano na Israel, baada ya wiki mbili za mashambulizi makali ambayo yamesababisha vifo vya watu 1,000 na kuwalazimisha wengine milioni moja kuyahama makazi yao.