1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wahofia vifo vya watoto Sudan

25 Agosti 2023

Umoja wa Mataifa umeonya kwamba vita na njaa vinaitishia nchi nzima ya Sudan ambako mamia kwa maelfu ya watoto wake wanaokabiliwa na utapiamlo wako katika hatari ya kufariki dunia.

https://p.dw.com/p/4VZcY
Sudan | Sudanesische Streitkräfte in Gadaref
Picha: AFP

Afisa mwandamizi katika Umoja wa Mataifa na mratibu wa misaada ya kiutu, Martin Griffiths, amesema, vita vya Sudan vinachochea hali kubwa ya dharura ya kiutu.

Sooma zaidi: Burhan aonekana kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, katika kipindi cha miezi minne iliyopita tangu mapigano ya Sudan yaanze, watu 5,000 wameuwawa na milioni 4.6 kulazimika kuyakimbia makaazi yao.