1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yahofia misaada baada ya uwanja wa ndege kushambuliwa

9 Machi 2023

Marekani imesema itakuwa na hofu iwapo uwasilishwaji wa misaada ya kiutu kwa wahanga wa tetemeko la ardhi nchini Syria utatatizwa kwa muda mrefu baada ya uwanja wa ndege wa Aleppo kushambuliwa kwa kombora la angani.

https://p.dw.com/p/4OQcc
Syrien Erdbeben l humanitäre Hilfsgüter am Flughafen in Aleppo
Picha: SANA/AP/picture alliance

Vyombo vya habari nchini Syria vimeinyoshea kidole cha lawama Israel kwa kombora hilo lililositisha huduma katika uwanja huo wa ndege.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, wizara ya uchukuzi ya Syria imezielekeza ndege zote zenye misaada ya wahanga wa tetemeko hilo la ardhi lililosababisha vifo vya maelfu ya watu, kutua Damascus au Latakia.

Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema, kufungwa kwa uwanja huo wa ndege huenda kukasababisha hali ngumu ya kiutu kwa wakaazi wa Aleppo ambalo ni mojawapo ya maeneo yaliyoathirika vibaya zaidi na tetemeko hilo la ardhi.

Haq amesema huenda Wasyria wengi wanaohitaji misaada ya kiutu mbali na Aleppo wakaathirika pia.