1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiItaly

UN: Wahamiaji walioingia Lampedusa wahamishwe

15 Septemba 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR limesema kuna umuhimu wa kuwahamisha maelfu ya wahamiaji waliowasili katika kisiwa kidogo cha Italia cha Lampedusa kutokana na uchache wa rasilimali kwenye kisiwa hicho.

https://p.dw.com/p/4WOEf
Polisi akiwa amesimama katikati ya wahamiaji walioingia Lampedusa na ambao wanasubiri kupelekwa kwenye maeneo mengine kutokana na uwezo mdogo wa kuwahifadhi
Polisi akiwa amesimama katikati ya wahamiaji walioingia Lampedusa na ambao wanasubiri kupelekwa kwenye maeneo mengine kutokana na uwezo mdogo wa kuwahifadhiPicha: Ciro Fusco/Ansa/picture alliance

Msemaji wa UNHCR Matthew Saltmarsch amesema wengi wa wahamiaji waliofika Lampedusa walikuwa wamechoka na kwamba wanahitaji chakula, malazi na huduma za matibabu.

Saltmarsh ameeleza kuwa ni vigumu kutambua sababu iliyopelekea wimbi hilo la wahamiaji kwenye kisiwa cha Lampedusa.

Takriban wahamiaji 7,000 wamewasili katika kisiwa cha Lampedusa katika muda wa siku mbili zilizopita.

Mamlaka ya Italia imehamisha idadi kubwa ya wahamiaji hao na kuwapeleka katika kisiwa chengine cha Sicily, huku kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi akisema anatarajiaa zoezi hilo kuendelea kwa siku zijazo.