1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Umoja wa Mataifa: Kuna baa la njaa Korea Kaskazini

18 Agosti 2023

Korea Kaskazini inaelezwa kuzidisha ukandamizaji wa haki za binadamu na raia wa taifa hilo wanazidi kukata tamaa na kuna pia ripoti za watu wanakufa kwa njaa baadhi ya maeneo ya nchi, huku hali ya uchumi ukidorora.

https://p.dw.com/p/4VJD1
Nordkorea l Kim Jong Un in einer Militärfabrik
Picha: KCNA via REUTERS

Hayo yamesemwa na Mkuu wa ofisi  ya Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk katika mkutano wa kwanza wa haki za binaadamu kuhusu Korea Kaskazini tangu mwaka 2017. Kiongozi huyo wa ofisi ya Umoja wa Mataifa amesema taarifa walizonazo ni kwamba watu wamekuwa na hofu ya kufuatiliwa na serikali, kukamatwa,kuhojiwa na kuwekwa kizuizini.

Kama mifano ya kuongezeka kwa ukandamizaji wa haki za binadamu, alisema, mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kufuatilia habari zenye maudhui ya  itikadi za kigeni na haswa kutoka Korea Kusini inawezekana akafungwa miaka 5 hadi 15 gerezani.

Watu wanapigwa risasi katika eneo la mpakani.

Türk amesema vikwazo vya serikali vimeongezeka zaidi, ambapo walinzi wamepewa mamlaka ya kumpiga risasi mtu yeyote anataka kuingia katika eneo ma mpakani bila ya ridhaa, ambapo kimsingi hadi wakati huu wageni wote wakiwemo maafisa wa Umoja wa Mataifa hawaruhusiwi kuingia katika mipaka ya ardhi ya Korea Kaskazini. zaidi anasema "Inakadiriwa kuwa maelfu ya Wakorea Kaskazini kwa sasa wako katika hatari ya kurejeshwa nchini kwao bila hiari, ambako wanaweza kuteswa, kuwekwa kizuizini kiholela au ukiukaji mwingine mkubwa wa haki za binadamu."

Katika sura ya suala la uchumi, serikali ya kwa sehemu kubwa imezipiga marufuku biashara na vyanzo vingine vya kujipatia kipato vya kibinafsi na kuendelea kufanya jitihada hizo kuwa ni uhalifu.

Taarifa ya baa la njaa Korea Kaskazini.

Nordkorea l Raktentest, Hwasong-18
Jaribio la kombora la masafa marefu la Korea KaskaziniPicha: File/KCNA via REUTERS

Kutokana na hali hiyo inaelezwa watu wengi wanakabiliwa na njaa na pia kuwepo kwa hali ngumu ya upatikanaji wa dawa.  Mkuu wa ofisi huyo  ya Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk anasema sehemu kubwa ya ukiukwaji wa haki za watu unatokana na jeshi la nchi hiyo.

Nae mchunguzi maalumu wa Umoja wa Mataifa, Elizabeth Salmón amesema watu wanakabiliwa na baa la njaa. Wengine wanakufa kutokana na utapiamlo, magonjwa na ukossefu wa upatikanaji huduma za afya.

Marekani na Korea Kaskazini, ambazo ziliingia vitani katika kipindi cha miaka ya 1950-53 katika kile kinachofahamika kama  Vita vya Korea, kimsingi bado zipo katika vuta nikuvute  tangu mzozo huo ulipomalizika. Mchunguzi Salmon anauita mzozo wa Marerkani na Korea wa Kaskazini kuwa ni mzozo mgando ambao kwa wakati huu unaendelezwa kwa kuoneshana nguvu za kijeshi.

Soma zaidi:Korea Kaskazini yajiandaa na majaribio ya makombora

Sera ya Korea Kaskazini ya "Jeshi Kwanza" inapunguza rasilimali kwa ajili ya watu, na viongozi wa nchi wanadai kwamba wao wabakaza mikanda yao ili fedha zitumike katika mipangop ya programu za nyuklia. Mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa yametakiwa kuongeza ufahamu wao katika mahusiano kati ya masuala ya haki za binaadamu huko Korea Kaskazini na amani na usalama wa kimataifa, na kulifanya taifa hilo liwajibike.