1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UMOJA WA MATAIFA NY:

10 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFtM
Katibu Mkuu wa Um Kofi Annan amesema leo kuwa watumishi wa Umoja huo wataendesha shughuli zao za kuisaidia Iraq kutoka kisiwani Cyprus kwavile Iraq bado ni hatari mno kwa UM kuanza upya karibuni shughuli zake nchini humo. Katika ripoti ya kurasa 26 kwa baraza la Usalama la UM,Katibu mkuu amesema misaada muhimu ya dhararua itaifikia Iraq kutoka sehemu mbali mbali katika eneo hilo.Annan alitangaza pia kuteuliwa kwa mjumbe wa muda wa Um kwa Iraq nae ni Mnew Zealand Ross Mountain. Maountain wakati huu ni m kuu wa afisi ya UM inayoongoza shughuli zake za kibinadamu mjini Geneva.Atakua makamo wa mkuu wa UM nchini Iraq atakeshika wadhifa uliokua mikononi mwa marehemu Baraza la utawala la Irak lililoteuliwa na Marekani linapanga kuunda M ahkama maalumu kuwashtaki wanachama wa utawala wa Saddam Hussein uliopinduliwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu.Wakuu wamearifu mahkama hiyo itaanzishwa rtasmi baadae hii leo.