1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa, New York. Umoja wa mataifa washtushwa na mashambulizi ya kinyama katika jimbo la Dafur.

9 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFP2

Umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika kwa pamoja wameshutumu vikali, shambulio la kinyama lililopangwa dhidi ya mji mmoja katika eneo la magharibi la jimbo la Dafur nchini Sudan lililofanywa na wanamgambo zaidi ya 350 wenye silaha wakati serikali ya nchi hiyo ikisitasita kutoa maeneo ambayo yatakaliwa na majeshi ya kulinda amani ya umoja wa Afrika ili kuzuwia matukio kama hayo.

Jan Pronk, mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa ,na balozi wa umoja wa Afrika Baba Gana Kingibe wamesema katika taarifa ya pamoja kuwa walipatwa na mshangao na mshituko mkubwa, baada ya kusikia kuhusu shambulio hilo la kinyama lililofanyika kwa siku nzima katika eneo la Khor Abeche lililofanywa na wanamgambo wa Miseriyya wa kabila la Niteaga.

Wanamgambo hao walifanya uharibifu mkubwa katika kijiji hicho, wakiuwa watu, kuchoma nyumba na kuharibu kila kitu wakiacha tu jengo la msikiti na shule.