1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa, New York. Serikali yakataa msaada wa fedha.

26 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEhj

Serikali ya rais Robert Mugabe imekataa kupokea dola za Kimarekani milioni 30 zilizotolewa na umoja wa mataifa ili kuwasaidia Wazimbabwe walioathirika na hatua ya serikali hiyo ya kuwavunjia nyumba zao za mabanda katika maeneo ya miji.

Mashirika ya misaada ya umoja wa mataifa yamewasilisha nyaraka kwa serikali wiki tatu zilizopita ambazo zitatoa msaada kwa watu zaidi ya 300,000, lakini hakukupatikana makubaliano, kwa mujibu wa mahojiano ya simu na maafisa wa mashirika ya misaada ya Afrika kusini ambao hawakutaka majina yao kutajwa.

Suala ni kwamba Zimbabwe haitaki kukubali kuwa inahitaji msaada na kuwa shabaha ya umoja wa mataifa katika kuipatia msaada wa dola milioni 30.

Serikali ya Zimbabwe haikufurahishwa na taarifa ya umoja wa mataifa ya Julai 22 ambayo imekiita kitendo cha serikali ya Zimbabwe kuvunja nyuma za mabanda mijini kuwa ni hatua ya kimaafa na isoyikubalika.