1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa-New-York: Muakilishi wa Ivory Coast katika umoja wa mataifa ametoa mwito

9 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFl0
kwa mara nyengine tena wa kutumwa kikosi cha umoja wa mataifa kusimamia amani katika nchi hiyo ya Afrika magharibi.Philippe Djangone-Bi,amesema wakati wa mkutano pamoja na waandishi habari mjini New-York ,ujumbe wa jumuia ya nchi za Afrika magharibi ulitiwa moyo na baraza la usalama la Umoja wa mataifa na Marekani ulipolizusha suala hilo mwaka jana.Muakilishi huyo wa kudumu wa Ivory Coast katika umoja wa mataifa anasema itakua bora zaidi kutumwa kikosi cha kulinda amani cha umoja wa mataifa badala ya wanajeshi wa Ufaransa au wa nchi jirani nchini humo.Kwa sasa umoja wa mataifa umetuma wachunguzi wachache tuu wa kiraia na maafisa wa kijeshi nchini Ivory Coast.