1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa mataifa , New York. Baraza kuu la umoja wa mataifa laukubali mkataba mpya dhidi ya ugaidi.

14 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNO

Baraza kuu la umoja wa mataifa limeunga mkono mkataba mpya wa ugaidi. Kama ukiidhinishwa utazilazimisha serikali zote kuwashitaki ama kuwapeleka katika nchi wanakotakiwa watu waliokamatwa na madini ya kinuklia ama vifaa vyake. Waraka huo ni wa 13 dhidi ya ugaidi na wa kwanza tangu shambulizi la kigaidi la Septemba 11 , 2001 dhidi ya Marekani. Unahitaji kuidhishwa na mataifa 22 ili kuwa sheria ya kimataifa.