1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa na Wakimbizi wa Kinyaruanda

10 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFEt

Geneva:

Umoja wa Mataifa umeonyesha wasiwasi wake leo kuhusu hatima ya Wanyaruanda elfu kadhaa waliokimbilia Burundi wakiogopa mahakama za „gacaca“. Mahakama hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuwahukumu watuhumiwa wa mauaji ya kiholela yaliyotokea mwaka 1994. Maafisa wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, wamesema kuwa Wanyaruanda wapatao 7,000 wamekimbilia Burundi tokea mwanzoni mwa mwezi uliopita wengi wao wakitishiwa kuuawa na kulipiziwa kisasi. UNHCR inawachukulia kuwa ni Wakimbizi hadi hapo hoja zao zitakapochunguzwa. Watuhumiwa wa mauaji ya halaiki wapatao zaidi ya 80,000 wako rumande wakisubiri kesi zao kusikilizwa. Wahutu wenye itikadi kali wamewaua Watutsi na Wahutu wenye itikadi za wastani Laki nane wakati wa mauaji hayo yaliyotokea mwaka 1994.