1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa: Mtanzania ateuliwa:

2 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFw9

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, amemteua aliyekuwa Mwanadiplomasia wa Tanzania, Daudi Mwakawago, kuwa Mjumbe wake maalumu nchini Sierra Leone. Anachukua wadhifa uliokuwa unashikiliwa na Oluyemi Adeniji, aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Nigeria. Mwakawago, aliyekuwa Waziri wa Habari na Utamaduni wa Tanzania, alikuwa pia Balozi wa nchi yake katika Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 1994 mpaka mapema mwaka huu.