1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNiger

Umoja wa Mataifa kusitisha safari za kibinadamu Niger

30 Desemba 2023

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limetahadharisha kwamba hivi karibuni linaweza kusitisha safari zake za ndege za kupelekea misaada ya kibinaadamu nchini Niger.

https://p.dw.com/p/4aizn
 WFP statement about looting of it´s  aid in Tigray
Nembo ya shirika la Mpango wa chakula dunianiPicha: Million Hailesilassie/DW

Hayo ni kutokana na ukosefu wa fedha huku jumla ya watu milioni 4.3 wakiwa wanahitaji msaada.

Katikati ya mwezi Novemba, shirika hilo la kimataifa lilitangaza kuanzisha tena safari zake katika nchi hiyo iliyokumbwa na mapinduzi ya kijeshi mnamo Julai 26 mwaka huu (2023), yaliyomuondoa madarakani rais aliyechaguliwa kidemokrasia, Mohamed Bazoum.

Mwakilishi na mkurugenzi wa WFP nchini Niger , Jean-Noel Gentile, amesema hali ya kifedha ya shirika la misaada la UNHAS tayari imeilazimisha kupunguza meli na ndege moja za kusafirisha misaada.

Mashirika mbalimbali ya misaada ya kimataifa kama WFP, UNHAS na OCHA wameelezea wasiwasi huo katika taarifa yao ya pamoja kutokana na ukosefu wa fedha na kutokuwa uhakika wa kupata ufadhili zaidi.