1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UMOJA WA MATAIFA: Katibu mkuu ataka tume ya kulinda amani Sierre Leone ifutiliwe mbali

6 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFG6

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa bwana Kofi Annan anataka tume ya kulinda amani ya Umoja huo nchini Sierre Leonne ifutiliwe mbali kwani kuna utulivu na usalama katika taifa hilo.

Katika ripoti yake aliyoiwasilisha kwa baraza la usalama la Umoja huo Annan amependekeza wanajeshi hao waanze kuondoka nchini humo kuanzia mwezi Agosti hadi desemba tarehe 31 mwaka huu.

Huku hali ya usalama ikiwa bado haijafikia kiwango cha kuridhisha na kwamba taifa hilo linahitaji msaada kutoka jamii ya kimataifa,Annan amesema hayo yanaweza kufikiwa na serikali ikishirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa na mataifa mengine na wala sio tume ya kulinda amani.