1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Afrika na hatua za kumaliza mapigano ya kikabila Sudan Kusini

18 Septemba 2020

https://p.dw.com/p/3ih0r

Balozi wa Umoja wa Afrika nchini Sudan Kusini Profesa Joram Biswaro amelihutubia baraza la usalama na amani la Umoja wa Afrika lenye nchi 15 kuhusu mapigano ya kikabila yanayoendelea Sudan Kusini na hatua ya kundi la wapiganaji wa National Salvation Front, NAS kukubali tena mwaliko wa Kanisa Katoliki nchini Italia kushiriki kwenye mazungumzo ya amani. Mwezi Januari mwaka 2020 kundi la NAS lilisaini mkataba wa amani mjini Rome, lakini limekataa kuitambua serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Sudan Kusini na limeendelea kufanya mashambulizi, ikiwemo tukio la hivi karibuni ambamo liliwauwa walinzi sita wa makamu wa rais. Sikiliza mahojiano yaliyofanywa na mwaandishi wetu Omar Mutasa na Balozi Biswaro.