1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yaahidi kuwa pamoja na ICC baada ya vikwazo vya Marekani

3 Septemba 2020

Umoja wa Ulaya umeahidi kushirikiana pamoja na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ya  ICC, dhidi ya jaribio la kuishusha hadhi yake, kwa Marekani kumwekea vikwazo mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo na afisa mwengine.

https://p.dw.com/p/3hxGp
Belgien EU-Haushaltsgipfel in Brüssel
Picha: Reuters/F. Lenoir

Taarifa ya kauli hiyo ya awali ipo katika andiko la msemaji wa Umoja wa Ulaya, ikiwa ni muendelezo wa majibu ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo ambae alitangaza vikwazo dhidi ya mwendesha mashtaka wa mahakama ya ICC yenye makao yake makuu mjini The Hague Uholanzi Fatou Bensouda na afisa mwingine waandamizi.

Afisa mwingine mwandamizi wa ICC, Phakiso Mochochoko anaguswa na vikwazo.

Bangladesch, Dhaka: Phakiso Mochochoko hält Pressekonferenz
Afisa mwandamizi ICC Phakiso MochochokoPicha: Getty Images/AFP/M. Zaman

Kwa mujibu wa taarifa ya Mwendesha mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda na afisa mwingine mwandamizi Phakiso Mochokochoko kwa pamoja wakabaliwa na vikwazo hivyo kwa kutokana na kuanzisha uchunguzi wa uhalifu wa kivita uliofanywa na wanajeshi wa Marekani katika operesheni zao nchini Afghanistan.

Kwa muda mrefu Marekani imekuwa ikiipinga ICC kutoa uamuzi wa kisheria dhidi ya hukumu kwa raia wa Marekani lakini, uamuzi wa mahakama hiyo kuchunguza  tuhuma za uovu uliofanyika Afghanistan umeuibua utawala wa Trump ambao umegeuka kuwa mpinzani wa taasisi hiyo.

Sauti ya Umoja wa Ulaya katika kuitetea ICC.

Msemaji wa Umoja wa Ulaya, katika ofisi ya Mkuu wa Sera za Kigeni Josep Borrel, Peter Stano anasema "Mahakama ya ICC inakabiliana na changamoto za nje za kupingwa na Umoja wa Ulaya unasimama imara dhidi ya majaribio ya kunyong'onyesha mifumo ya kimataifa kufanikisha haki ya jinai kwa kuzuia utendaji kazi wake".

Soma zaidi:HRW: Marekani yamuwekea vikwazo Bensouda

Aidha akielezea zaidi wakati alipozungumza na waandishi wa habari alisema umoja huo umejiweka madhubuti kuongeza uungaji mkono wao kwa ICC kwa sababu hiyo ni nyenzo muhimu katika makabiliano ya wakwepa mikono ya sheria. Katika hatua nyingine, Msemaji wa ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza ametangaza kuwa Uingereza vilevile imesikitishwa na hatua iliyochukuliwa na Marekani dhidi ya maafisa wa ICC.

Awali Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Mike Pompeo iliipuuza mahakama hiyo kwa kuiita "Mahakama ya Kangaroo" akidai ina namna yake kuendesha uchunguzi wa madai ya tuhuma dhidi ya vikosi vya Marekani.

Chanzo: AFP