1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yaziwekea vikwazo kampuni zinazochangia vita Sudan

22 Januari 2024

Baraza la Umoja wa Ulaya hii leo limeidhinisha vikwazo dhidi ya kampuni sita zinazojihusisha na vita vya nchini Sudan, ambako vikosi vya serikali na wanamgambo wa RSF wanapigana tangu Aprili 2023.

https://p.dw.com/p/4bYIQ
Sudan | Rapid Support Forces
Wapiganaji wa kikosi cha RSF nchini Sudan.Picha: Hussein Malla/AP Photo/picture alliance

Baraza hilo limesema kwenye taarifa kwamba kampuni hizo sita zilikuwa zikihusika na kuunga mkono shughuli zilizodhoofisha utulivu na mabadiliko ya kisiasa nchini Sudan.

Kampuni mbili kwenye orodha hiyo zinajihusisha na uzalishaji wa silaha na magari ya kijeshi kwa ajili ya jeshi la Sudan, SAF, na matatu zinazofanya manunuzi ya vifaa vya kijeshi kwa ajili ya RSF. 

Baraza hilo limesema mali za kampuni hizo zitazuiwa na hazitaruhusiwa kutoa ufadhili kwa ajili yao ama kwa ajili ya maslahi yao.