1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Umoja wa Ulaya wazidi kuibinya Urusi kwa vikwazo

27 Mei 2024

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Brussels leo wameamua kuiwekea vikwazo Huduma ya Magereza ya Urusi na Warusi wengine 19 kwa ukiukaji wa haki za binadamu

https://p.dw.com/p/4gLUG
Waandamanaji nchini Ujerumani wakiwa wamepiga kambi kuipinga Kremlin, kufuatia kifo cha Navalny
Picha ya aliyekuwa mpinzani mkuwa wa Rais Vladimir Putin wa Urusi Alexei Navalny Picha: Paul Zinken/ZB/dpa/picture alliance

Katika taarifa, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema kifo cha Navalny ni ishara nyingine inayoonesha ukandamizaji unaofanywa na serikali ya Urusi.

Vikwazo hivyo vinawajumuisha majaji wa Urusi, waendesha mashtaka na maafisa wa idara ya mahakama ambapo iwapo wana mali zozote katika Umoja wa Ulaya basi zitafungiwa na kampuni za Ulaya hazitakiwi kuwapa fedha.

Watu hao 19 pia hawawezi kuingia wala kusafiri kupitia nchi za Umoja wa Ulaya. Kremlin imekanusha kuhusika kivyovyote vile kwa serikali ya Urusi katika kifo cha Navalny.