1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya kuwa na app ya kufuatilia corona

17 Aprili 2020

Nchi za Ulaya zinatengeneza app maalum za kufuatilia virusi vya Corona na Umoja wa Ulaya umezitolea mwito nchi wanachama wake 27 wakati zinapotengeneza app hizo zifikirie kuzifanya ziwe ni za kutumika kwa khiyari.

https://p.dw.com/p/3b4ZM
Coronavirus App Infektionszahlen Europa Welt  / Zahlen für Illustration manipuliert
Picha: picture-alliance/xim.gs

Nchi za Ulaya zinatengeneza app maalum za kufuatilia virusi vya Corona na Umoja wa Ulaya umezitolea mwito nchi wanachama wake 27 wakati zinapotengeneza app hizo zifikirie kuzifanya ziwe ni za kutumika kwa khiyari na kuhakikisha kwamba mifumo ya mataifa mengi inaweza kufanya kazi kwa pamoja.

Watu zaidi ya 850,000 wameambukizwa virusi hivyo vya Corona na kiasi 90,000 wamefariki kwa mujibu wa kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Umoja wa Ulaya.

Wakati nchi zikianza kuondowa marufuku za kuzuia watu kutembea,suala la kufuatilia ikiwa mtu amekutana na aliyeambukizwa virusi hivyo litakuwa muhimu zaidi ili kufungua fursa ya maisha ya kawaida kurejea.

Europäisches Parlament Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri kuu ya Ulaya, Ursula von der LeyenPicha: Getty Images/AP/K. Tribouillard

Matumizi ya Apps za Corona.

Matumizi ya apps kama hizo yataondowa ulazima wa shughuli inayochukuwa muda mrefu ya kuwahoji watu chungunzima ambao wameambukizwa virusi hivyo ili kujaribu kubaini hasa walikovipata virusi hivyo.

Katika muongozo wa mwanzo kabisa,Halmashauri ya Umoja wa Ulaya inasema kwamba imani ya wananchi ni muhimu zaidi kwa mfumo huu kufanya kazi kwasababu apps hizo zinazotengenezwa zitakuwa za uhakika ikiwa watu watazitumia.

Msemaji wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Johannes Bahrke amesema apps hizo zinaweza tu kuonesha mafanikio kamili ikiwa watu watazitumia na kwa hivyo Umoja wa Ulaya unataka kuwapa wananchi wake apps watakazoziamini.

Griechenland Athen unbegleitete minderjährige Flüchtlinge reisen nach Luxemburg und Deutschland
Upo wasiwasi iwapo App hiyo itatumika kwa hiyari, ikimaanisha wengi hawatapimwa Picha: AFP/O. Panagiotou

Wasiwasi uliopo.

Kadhalika Bahrke ameweka wazi kwamba ni kitu cha msingi kwamba hatua ya kuwa na app hiyo na matumizi yake iwe ni kwa khiyari.

Wasiwasi umekuwa ukiongezeka kuhusu uwezekano wa uwezo wa kufuatiliwa kwa nyendo za watu au hatari ya kwamba data za watu huenda zikasambazwa na watu wasiojulikana bila ya ridhaa zao.

17.04.2020 Matangazo ya Mchana

Katika kipindi cha miaka kadhaa sasa mashirika ya kutetea watumiaji bidhaa ya Ulaya yamekuwa yakiwaonya watu kuhusu hatari ya taarifa zao kujulikana,inayosababishwa na matumizi ya vifaa vya mtandaoni vya kufuatilia afya.

Kwa maana hiyo Halmashauri ya Ulaya inasema majukwaa hayo yanapaswa kusimamiwa na mamlaka za afya ya umma na kuondolewa pale wakati ukifika yakiwa hayahitajiki tena.

Msisitizo unaotolewa ni kwamba apps hizo ziwe za hiyari kwa wanaotaka kuzipakua,na watu hawapaswi kuadhibiwa ikiwa wataamua kutopakua apps hizo.

Mashirika: APE

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW