1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine:Urusi inapanga kutengeneza ajali Zaporizhzhia

27 Mei 2023

Wizara ya Ulinzi nchini Ukraine imesema Urusi inapanga kutengeneza ajali kubwa katika kituo cha nguvu za nyuklia Zaporizhzhia kinachodhibitiwa na vikosi vinavyounga mkono Moscow.

https://p.dw.com/p/4Rt40
Ukraine | Atomkraftwerk Saporischschja
Picha: Andrey Borodulin/AFP/Getty Images

Wizara hiyo ya  Ulinzi ya Ukraine imesema Urusi inapanga kkufanya hivyo ili kujaribu kuzuia uvamizi wa Ukraine uliopangwa kwa muda mrefu ukilenga kutwaa tena eneo hilo la kimkakati.

Idara ya kijasusi ya wizara hiyo imesema kwamba hivi karibuni vikosi vya Urusi vitashambulia mtambo huo na kutangaza kuvuja kwa mionzi hatua ambayo italazimisha uchunguzi wa mamalaka za kimataifa na kusitishwa kwa uhasama kwa pande zote.

Shirika la Kimataifa la Kudhibiti nishati ya Atomiki IAEA lenye makao yake mjini Vienna ambalo mara zote limekuwa likifuatilia shughuli katika mtambo huo na kutoa taarifa, bado halijatoa kauli yoyote kuhusiana na tuhuma hizo zilizotolewa na Ukraine dhidi ya Urusi.