1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yazima shambulizi jingine la Urusi mjini Kyiv

20 Mei 2023

Mifumo ya ulinzi ya Ukraine imezima shambulizi jingine kubwa la Urusi kwa kuzindungua droni kadhaa zilizolenga kuushambulia mji mkuu wa taifa hilo, Kyiv, usiku wa kuamkia leo.

https://p.dw.com/p/4RbVh
Droni ya Urusi
Droni ya Urusi Picha: AFP

Taarifa iliyotolewa na jeshi la anga la Ukraine imesema zaidi ya droni 18 zinazoaminika kuwa zimeundwa nchini Iran zilidunguliwa juu ya anga ya mji wa Kyiv na nyingine 20 ziliangushwa kwenye maeneo tofauti ya Ukraine.

Mamlaka za mji huo mkuu zimesema mabaki yaliyoanguka ya zana hizo za kivita yamesababisha uharibifu wa majengo kadhaa, magari na miundombinu ya barabara lakini hakuna hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha.

Hiyo itakuwa ni mara ya 11 kwa Urusi kuulenga mji wa Kyiv tangu mwanzoni mwa mwezi Mei lakini hujuma hizo hazifanya uharibifu mkubwa kutokana na kuimarika kwa mifumo ya ulinzi ya Ukraine.