1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yaitisha mkutano wa Baraza la Usalama la UN

26 Machi 2023

Ukraine imetoa wito hii leo wa kufanyika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatia tangazo la Urusi kwamba itapeleka silaha za nyuklia nchini Belarus.

https://p.dw.com/p/4PGYb
Dmytro Kuleba Außenminister Ukraine
Picha: Volodymyr Tarasov/Avalon/Photoshot/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba amesema Kyiv inatarajia hatua madhubuti kutoka kwa Marekani, Uingereza, China na Ufaransa ili kukabiliana na vitisho vya nyuklia  vya Urusi.

Soma pia: Ukraine: Urusi inaishikilia Belarus kama “mateka wa nyuklia“

Nayo Jumuiya ya Kujihami ya NATO imeikosoa kauli ya rais wa Urusi Vladimir Putin na kusema ni kauli ya hatari na ya kutowajibika na kusema wako makini na wanafuatilia kwa karibu hali hiyo. Urusi imekuwa ikivunja mara kwa mara ahadi zake za udhibiti wa silaha.