1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yashutumu Urusi kwa kufanya mashambulizi mabaya

18 Mei 2023

Ukraine imesema mji wake mkuu Kiev, umekabiliwa na mashambulizi ya angani "yasiyokuwa ya kawaida” mapema leo.

https://p.dw.com/p/4RXg7
Ukraine Krieg | Raketenangriff auf Kiew
Picha: National Police of Ukraine/REUTERS

Makubaliano hayo ambayo ni ishara ya nadra, ya ushirikiano, kati ya pande hizo mbili hasimu, yalikaribishwa na Umoja wa Mataifa na vilevile Marekani.

Hata hivyo kuna hofu kuhusu kudumu kwa mkataba huo, kufuatia madai ya Ukraine kwamba Urusi imefanya mashambulizi yasiyokuwa ya kawaida dhidi yake mjini Kiev na katika maeneo mengine.

Jeshi la Ukraine limesema liliangusha makombora 29 kati ya mengine 30 yaliyofyatuliwa na Urusi usiku wa kuamkia leo, lakini mtu mmoja aliuawa katika mji wa kusini Odesa.