1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Ukraine yaanzisha uchunguzi kuhusu wanajeshi wake wawili

3 Desemba 2023

Ukraine imeanzisha uchunguzi kuhusu kile ilichosema ni "mauaji'' yaliofanywa na vikosi vya Urusi ya wanajeshi wake wawili ambao hawakuwa na silaha

https://p.dw.com/p/4Zj6e
Wanajeshi wa Urusi katika hafla ya kuadhimisha miaka 78 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia Mei 9, 2023,
Wanajeshi wa UrusiPicha: Alexander Zemlianichenko/AP

Siku ya Jumamosi (3.12.2023) video fupi ambayo uhalisi wake haukuweza kuthibitishwa na shirika la habari la AFP na iliyochapishwa katika mtandao wa kijamii wa Instagram, ilionesha wanaume wawili wakitoka kwenye jengo moja, mmoja akiwa ameweka mikono yake juu ya kichwa chake kabla ya kulala chini mbele ya kundi jingine la wanajeshi.

Wanajeshi hao walifyetua risasi na kilichofuatia hakikuonekana.

Ukraine yalaani mauaji hayo na kuyataja kuwa ''uhalifu wa kivita''

Kituo cha mawasiliano ya kimkakati cha Ukraine, kimedai kuwa na taarifa zilizothibitishwa zinazosema video hiyo ilionesha mauaji hayo yalifanywa na wanajeshi wa Urusi dhidi ya wanajeshi wa Ukraine ambao hawakuwa wamejihami kwa silaha. Mchunguzi wa haki za binadamu wa Ukraine Dmytro Lubinets, amelaani tukio hilo alilolitaja kuwa "uhalifu wa kivita."

Hata hivyo hadi sasa bado hakuna majibu rasmi kutoka Urusi.