1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yaituhumu Urusi kwa kuyashambulia maghala yake

19 Julai 2023

Ukraine imeituhumu Urusi leo kwa kuyashambulia makusudi maghala yake ya nafaka katika bandari za Bahari Nyeusi na kuharibu tani nyingi za chakula.

https://p.dw.com/p/4U8Hb
Ukraine I Volodymyr Selenskyj
Picha: Sergei Supinsky/AFP

Hii ni tangu Moscow ilipojiondoa katika mkataba wa usafirishaji nafaka uliokusudia kuepusha mgogoro wa kimataifa. Tuhuma hizo za Kyiv zimejiri huku moto usiojulikana chanzo chake ukiteketeza kituo cha kijeshi katika rasi ya Crimea iliyokwapuliwa na Urusi. Hali hiyo ililazimisha maafisa wa eneo hilo kuwahamisha zaidi ya wakaazi 2,000.

Rais wa Ukraine asema nchi hiyo inajenga njia ya meli ya muda

Urusi iliyapiga maeneo ya Odesa kwa usiku wa pili mfululizo. Rais Volodymyr Zelensky amesema Ukraine inajenga njia ya meli ya muda ili kuendeleza mchakato wa usafirishaji wa nafaka baada ya Urusi kujiondoa kwenye makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa kupitia ujia salama wa Bahari Nyeusi. Kyiv imedai Urusi iliharibu tani 60,000 za nafaka iliyokusudiwa kusafirishwa, katika mashambulizi ya usiku kucha karibu na mji wa bandari wa Odesa.