1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine yasema kijiji kimoja kimekombolewa upande wa kusini

19 Juni 2023

Naibu Waziri wa Ulinzi Ganna Maliar amesema vikosi vya Ukraine vimechukua tena udhibiti wa kijiji cha Pyatykhatky upande wa kusini,

https://p.dw.com/p/4SkTG
Russland - Ukraine - Konflikt
Picha: Efrem Lukatsky/AP/picture alliance

Naibu Waziri wa Ulinzi Ganna Maliar amesema vikosi vya Ukraine vimechukua tena udhibiti wa kijiji cha Pyatykhatky upande wa kusini, na kusisitiza kuwa jumla ya maeneo manane yamekombolewa mwezi huu tangu kuanza kwa mashambulizi yake ya ukombozi.

Soma pia: Urusi huenda ilihusika na hujuma za Kakhovka

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema hivi leo kuwa vikosi vyake vimezuia jaribio la Ukraine la kutaka kuchukua udhibiti wa kijiji cha Novodonetske katika mkoa wa mashariki wa Donetsk, na kwamba wameharibu magari ya kivita ya Ukraine.

Wakati huo huo, Shirika la kijasusi la Urusi (FSB) limesema limefanikiwa kuzuia msururu wa kile ilichokiita "hujuma na njama za kigaidi" za Kiev zinazolenga maafisa wanaoungwa mkono na Moscow katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi nchini Ukraine.

AFP