1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Jeshi la Ukraine ladai kuharibu mifumo ya ulinzi ya Urusi

10 Juni 2024

Jeshi la Ukraine limedai kuharibu mifumo ya ulinzi wa anga na ardhini ya Urusi katika mashambulizi ya makombora ya usiku kucha katika eneo la rasi ya Crimea inayokaliwa na Moscow.

https://p.dw.com/p/4gsd3
Ukraine | Vita | Rais Zelensky
Rais Volodymyr Zelensky akimtunuku mmoja wa maafisa wa jeshi la nchini Ukraine katikati ya vita vinavyoendelea kati yao na UrusiPicha: Ukrainian Presidency/ZUMA Wire/IMAGO

Kulingana na jeshi hilo mashambulizi hayo yalifanyika katika eneo la Dzhankoi, ambako yalisababisha "hasara kubwa" kwa ulinzi wa anga wa Urusi.

Hata hivyo, madai hayo hayakuweza kuthibitishwa mara moja na hakukuwa na maoni yoyote kutoka kwa wizara ya ulinzi Urusi.

Urusi imevurumisha mara kwa mara makombora ya masafa marefu kusini mwa Ukraine kutoka rasi ya Crimea ambayo Moscow waliikamata na kuidhibiti mwaka 2014.